Tangazo la Shiwata created by innowise(Banners)



Monday, January 20, 2014

Shiwata yaizawaidia Kampuni ya Issere Sports

Na Peter Mwenda

KAMPUNI ya Issere Sports inayojishughulisha na uuzaji wa vifaa vya michezo nchini ni miongoni mwa wanamichezo, wasanii na awaandishi wa habari 1,000 waliotunukiwa vyeti vya utendaji bora katika fani za michezo kwa mwaka 2013 hadi 2014 katika kongamano lililofanyika ukumbi wa Lamada, Ilala Dar es Salaam.

Katika kongamano hilo ambalo kulitolewa mada mbili za kusaidia jamii ya michezo kuepuka matumkizi ya dawa za kulevya na kuwa na maadili mazuri katika jamii, Kampuni ya Issere ni pekee iliyopata nafasi ya kuwakilisha nyingine zinazojihusisha na uuzaji wa vifaaq vya michezo.

Mkurugenzi wa Masoko wa Issere Sports, Abbas Issere aliyepokea vyeti hivyo kwa niaba ya wanamichezo wengine wa Kampuni hiyo alisema zawadi hiyo ni changamoto kwa wanamichezo kushirikiana pamoja badala ya kubaguana kurejesha heshima katika michezo kama ilivyokuwa zamani.

Kampuni ya Issere Sports ambayo imeingia mkataba wa kuuza jezi za Klabu ya Simba, imekuwa ikiuza na kusambaza jezi hizo nchini katika mashirika ya umma, Wizara, Halmashauri za Wilaya na mashuleni katika ngazi ya shule za msingi, Sekondari nas vyuoni.

No comments:

Post a Comment

Advertising Here