Wanachama 70 kwenda Mkuranga Jumapili
Na Mwandishi Wetu
MTANDAO wa wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa safari ya wasanii wapatao 70 kwenda Mkuranga kwa ajili ya kuoneshwa maeneo yao.
Katibu wa SHIWATA, Selemani Pembe alisema safari hiyo itaanzia kwenye ofisi za Mtandao huo Bungoni zilipo ofisi za Splendid siku ya Jumapili, Juni 2, 2013.
Pembe alisema wanachama wanaokwenda Mkuranga wafike saa 2 asubuhi na watakaochelewa hawasubiriwa.
Alisema mpaka sasa SHIWATA imejenga nyumba 20 kati hizo zipo zilizosubiri kukombolewa za gharama ya sh. mil. 7,300,000, sh. mil. 6,600,000 na sh. 619,000 zilizokandikwa kwa udongo na kuezekwa kwa bati.
mwisho
No comments:
Post a Comment