Tangazo la Shiwata created by innowise(Banners)



Wednesday, June 18, 2014

Saturday, June 14, 2014

PICHA ZA MAZIKO YA BONDIA MAREHEMU IRAQ HUDU 'MKUMWENA' ALIVYOZIKWA KATIKA MAKABURI YA KISUTU


Jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Iraq Hudu 'Mkumwena' wakipeleka mwili kuzika katika makaburi ya Kisutu Dar es salaam kwa ajili ya kumuhifadhi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya waombelezaji wakitia udongo katika kaburi la marehemu Iraq Hudu wakati wa maziko yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kisutu Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya waombelezaji na mabondia wakiwa nyumbani kwa marehemu Iraq Hudu kutoka kushoto ni bondia Adwer George, Rashidi Matumla, Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini Yasini Abdallah na Mwenyekiti wa Shiwata Cassim Twalibu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mtoto wa Marehemu Iraq Hudu, Daniel Hudu  kushoto akisalimiana mabondia Adrwe George,Rashidi Matumla na Rais wa TPBO Yassin Abdallah
Mtoto wa Marehemu Iraq Hudu, Daniel Hudu  kushoto akisalimiana mabondia Adrwe George,Rashidi Matumla na Rais wa TPBO Yassin Abdallah
Mashekhe wakisoma duwa kabla ya kwenda kuzika
Meneja wa bendi ya msondo ngoma Said Kibiriti akisalimiana na mabondia
Baadhi ya waombelezaji waliojitokeza
Mtangazaji Maulid Baraka Kitenge akizungumza na mabondia mbalimbali wakati wa msiba wa bondia Iraq Hudu
Mtangazaji wa kipindi cha Michezo Maulid Baraka Kitenge akisalimiana na bondia mkongwe ambaye kwa sasa ni kocha wa MKoa wa Tanga katika wilaya ya Muheza Chales Muhilu 'Spins'
Bondia Marehemu Iraq Hudu 'Kimbunga' kulia enzi za uhai wake katikati ni marehemu bondia Papa Upanga
Bondia Iraq Hudu' Kimbunga kulia akipambana na Stanley Mabesi katika mpambano wao
IRAQ HUDU
WAOMBWELEZAJI WAKIWA WAMEBEBA JENEZA LA MAREHEMU IRAQ HUDU
WAOMBWELEZAJI WAKIWA WAMEBEBA JENEZA LA MAREHEMU IRAQ HUDU
Mmoja wa waombelezaji kulia akimpa pole bondia Chuku Duso katika msiba wa bondia Iraq Hudu
Ibrahimu Kamwe na Said Chaku
wadau mbalimbali wa mchezo wa ngumi
WAOMBWELEZAJI WAKIWA WAMEBEBA JENEZA LA MAREHEMU IRAQ HUDU


WAOMBELEZAJI WAKITIA UDONGO KWENYE KABURI LA MAREHEMU IRAQ HUDU
WAOMBELEZAJI WAKITIA UDONGO KATIKA KABURI LA IRAQ HUDU
WAOMBELEZAJI WAKITIA UDONGO KATIKA KABURI LA IRAQ HUDU PICHA NA www.superdboxingcoach.blogspot.com

SHIWATA yagawa mashamba kwa wanachama wake

MTANDAO WA WASANII TANZANIA                 (SHIWATA)

          PRESS RELEASE

SHIWATA imeamua kutoa ofa ya kugawa shamba lake la ekari 500 lililoko Mkuranga mkoa wa Pwani kwa wanachama wake wenye uwezo wakulima mazao mbalimbali yatakayochangia kupunguza uhaba wa chakula nchini.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mwenyekiti wa Mtandao wa SHIWATA, Cassim Taalib kwa vyombo vya habari inasema wanachama watakaogaiwa shamba hilo ni wale walio hai walio lipia ada zao watapaswa kutoa sh. 200,000 kulipia ekari moja atakayopewa.

Alisema kuratibu mpango huo SHIWATA imeitisha mkutano wa wanachama wote Jumamosi Juni 21,2014 kwenye ukumbi wa Splendid Ilala ili kujadili mambo mbalimbali katika kijiji cha wasanii Mkuranga ambacho mpaka sasa kimejenga na kukabidhi nyumba 66 kwa wanachama wake kati ya 265 wanaojenga nyumba zao kwa njia ya kuchangishana.

"Ujenzi wa nyumba za kisasa katika kijiji chetu cha Mwanzega Mkuranga chenye ukubwa wa hekari 300 unaendelea tunatarajia kukabidhi nyumba 40 Desemba mwaka huu katika sherehe kubwa ambayo tunatarajia kumpata mgeni rasmi kutoka ngazi za juu" alisema Mwenyekiti.

Alisema shiwata inawataka wanachama wote ambao hawakuwahi kwenda kuona au kukabidhiwa viwanja au nyumba zao kutokana na sababu mbalimbali wafike na kadi zao ofisini Ilala Bungoni Chuo cha Splendid kabla ya Jumatano Juni 19, 2014 ili wakakabidhiwe nyumba zao na kiwanja vyao Jumamosi Juni 21, 2014 saa 2 asubuhi kwa nauli ya sh. 10,000 ya kwenda na kurudi.

Aliwatoa wasiwasi wanachama waliokuwa wanahofia kuwekeza katika ujenzi wa nyumba kuwa mpango wa kupimia wasanii nyumba zao ili wapate fursa ya kukopa kutoka benki mbalimbali za hapa nchini umeanza kushirikiana na Idara ya Ardhi ya Halmashauri ya Mkuranga ikifuatiwa na ujenzi wa barabara, uvutaji wa umeme na uchimbaji visima vya kisasa unafanyiwa kazi.

Aliwahimiza wanachama wanaochangia ujenzi wa nyumba zao kukamilisha michango hiyo ili wakabidhiwe nyumba zao kukamilisha malengo ya kuwasaidia wasanii kujikwamua kiuchumi.

Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) ulianzishwa mwaka 2004 na kusajiliwa na baraza la sanaa tanzania shiwata mwaka 2005 pia imesajiliwa na brella kwa shughuli za kiuchumi ikiwa na dira ya kuwakomboa wasanii kuwa na maisha bora kupitia mtandao huu ifikapo mwaka 2015.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Ofisa Habari wa SHIWATA, Peter Mwenda 0715/0752 222677.

mwisho.

Tuesday, June 10, 2014

Mwili wa Marehemu Gebbo Peter waagwa nyumbani kwake Vingunguti,Kuzikwa kijijini kwao Kigurunyembe mkoani Morogoro





Sehemu ya wachezaji mpira wa sasa na wazamani wakiwa wamesimama pembeni ya Jeneza lenye Mwili wa aliyekuwa Mchezaji wa Timu ya Simba miaka ya nyuma,Marehemu Gebbo Peter aliefariki jana kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.hapa wakiwa nyumbani kwake Vingunguti tayari kwa safari ya kwenda kwenye maziko yake Kigurunyembe mkoani Morogoro (Picha na Evance Ng'ingo)

Wadau mbali mbali wa soka wakiwemo viongozi wa soka wakipita kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Marehemu Gebbo Peter,Nyumbani kwake Vingunguti,jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza safari ya kuelekea Kigurunyembe mkoani Morogoro kwa mazishi.
Ibada ikifanyika.
Mbunge wa Jimbo la Ilala,Mh. Mussa Azzan Zungu akitoa heshima za Mwisho.

Mwili ukiwasili nyumbani.
Older Post

Thursday, June 5, 2014

Mkuu wa Wilaya Mkuranga, Mercy agawa nyumba

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila akizungumza kwenye sherehe za kukabidhi nyumba kwa wasanii katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga.

Viongozi wa juu Basata ndani ya kijiji cha wasanii Mkuranga

Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Profesa Penina Mlama akiwa na Katibu wake Mtendaji, Godfrey Mungereza wakijadiliana katika kijiji cha wasanii Mkuranga.

Advertising Here